Thursday, 23 April 2015

SENGA: Busu la Kajala Lanilaza Usingizi Mnono

Thursday, 23 April 2015 - by Unknown 0


Mchekeshaji maarufu Bongo, Joseph Senga ‘Senga’ amefunguka kuwa busu alilompiga staa wa kike wa filamu, Kajala Masanja lilimfanya alale usingizi mnono sana ukizingatia kuwa hajawahi kubusu shavu laini kiasi hicho kwasababu warembo wengi wanazingua.

Akizungumza na Centre Spread, Senga alisema alipata fursa hiyo ya kumpiga busu wakati wakiigiza filamu matata ya Pishu iliyoandaliwa na Kajala Entertainment, itakayoingia sokoni Mei Mosi, ambapo alisema anajikubali katika filamu hiyo ambayo anaamini itavunja watu mbavu.
 
“Wewewee umpige busu Kajala utashindwa kulala kweli jamani,yaani nilishtuka kumeshakucha kabisa lakini pamoja na yote mimi ni mchekeshaji ila kwa filamu ya Pishu nimeinua mikono,” alisema Senga.
 

TAZAMA TRAILER YA FILAMU MPYA YA PISHU - KAJALA ENTERTAINMENT PRESENTS, KUWA MADUKANI KUANZIA TAREHE 1.05.2015 

Tags:
About the Author

Write admin description here..

0 comments:

© 2015 THE CIRCLE TV.