Friday, 24 April 2015

PICHA: POLISI ANUSURIKA KUUAWA KWA KIPIGO CHA WANANCHI MOROGORO

Friday, 24 April 2015 - by Unknown 0


Askari mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria , aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, amenusurika kuuawa jana mchana na wananchi wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva wa bodaboda ambaye aliparamia lori.

Tukio hilo linawahusisha askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU ) waliokuwa wakiendesha pikipiki yenye namba za usajili za PT 823 ambayo ni mali ya polisi .

Mashuhuda wamesema kwamba polisihaowalikuwa wakimfukuza dereva huyo wa bodaboda ambaye alikwenda kujikita katika lori ambapo wananchi waliwatuhumu kusababisha ajali hiyo na kuanza kuwashambulia.

Baada ya kuona hivyo , polisi hao walianza kurusha risasi hewani lakini wananchi waliwakabili kwa kuwarushia mawe na hivyo  umjeruhi polisi mmoja.

About the Author

Write admin description here..

0 comments:

© 2015 THE CIRCLE TV.