LATEST POST

    Wednesday, 17 June 2015

    Mama Mzazi: Banza Stone yuko Hoi, Haongei, Amegoma kula Kula na Kunywa dawa, wasanii Wamemtenga

    IMG_8689

    Mama mzazi wa muimbaji wa muziki wa dance, Banza Stone amesema mwanae afya yake imezidi kuzorota na sasa amegoma kula chakula wala kunywa dawa.

    Akiongea na Ripoti ya kipindi cha Ubaoni cha EFM juzi, mama huyo alisema hadi siku hiyo Banza alikuwa amegoma kula kwa siku tatu mfululizo.

    Aliongea kuwa pamoja na kuugua hivyo bado wasanii wenzake wameshindwa kwenda kumjulia hali.
    “Mpaka sasa sijamuona mtu yeyote aliyekuja kumshughulikia na kumwangalia, wamemwacha hivi hivi. Na mimi siwezi kuwalaumu kwanini hamjaja kumwangalia, kila mtu na moyo wake, mwenye kuja atakuja, mimi ntahangaika na mtoto wangu mpaka pale atakapoamua mwenyezi Mungu,” alisema Mama Banza.

    Kwa mujibu wa kaka yake, Banza, Jabir Masanja, anasumbuliwa na fangasi kichwani mwake na dawa anazotumia ni kali kiasi cha kumpotezea hamu ya kula.

    Jabir amewaomba wadau wa muziki na mashabiki wake walioguswa kumchangia chochote Banza kwa kutuma chochote kutumia namba: 0715407088 au 0753786016.
    more »

    Sunday, 3 May 2015

    PICHA ZA MATUKIO YA ZIARA YA WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI DSJ KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM


    kabla ya kuanza safari matukio tofauti ya upigaji wa picha mbalimbali yakiendelea

    kameraman naye hakuwa mbali kwenye picha za mapozi ya kizamani

                               upigaji wa picha uliendelea zaidi

    hapa mahojiano na baadhi ya wanachuo yalianza rasmi


    safari ilianza rasmi

    baada ya safari kuanza

    walipowasili kituoni hapo

    mkuu wa msafara akiweka sahihi katika kitabu cha wageni

    kiongozi wa serikali ya wanachuo akisaini

    mwenyeji wa kituo akitoa maelekezo


                                 furaha iliendelea zaidi na kufurahia na watoto

                             mmoja wa wahudumu wa afya wa kituo akitoa maelekezo
                                 kameraman wetu akiwa kazini
                                  watoto wakitoa shukrani
                                         mahojiano yaliendelea

    baadhi ya vitu walivyojitolea


    wakiwa na mmoja wa waandishi wa habari
    PICHA ZOTE KWA HISANI YA THE CIRCLE ONLINE TV
    more »

    Saturday, 2 May 2015

    MAYWEATHER ATWAA UBINGWA KWA KUMTANDIKA PACQIAO >>>>TAZAMA HAPA





    more »

    Friday, 24 April 2015

    PICHA: POLISI ANUSURIKA KUUAWA KWA KIPIGO CHA WANANCHI MOROGORO


    Askari mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria , aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, amenusurika kuuawa jana mchana na wananchi wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva wa bodaboda ambaye aliparamia lori.

    Tukio hilo linawahusisha askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU ) waliokuwa wakiendesha pikipiki yenye namba za usajili za PT 823 ambayo ni mali ya polisi .

    Mashuhuda wamesema kwamba polisihaowalikuwa wakimfukuza dereva huyo wa bodaboda ambaye alikwenda kujikita katika lori ambapo wananchi waliwatuhumu kusababisha ajali hiyo na kuanza kuwashambulia.

    Baada ya kuona hivyo , polisi hao walianza kurusha risasi hewani lakini wananchi waliwakabili kwa kuwarushia mawe na hivyo  umjeruhi polisi mmoja.

    more »

    Thursday, 23 April 2015

    SENGA: Busu la Kajala Lanilaza Usingizi Mnono


    Mchekeshaji maarufu Bongo, Joseph Senga ‘Senga’ amefunguka kuwa busu alilompiga staa wa kike wa filamu, Kajala Masanja lilimfanya alale usingizi mnono sana ukizingatia kuwa hajawahi kubusu shavu laini kiasi hicho kwasababu warembo wengi wanazingua.

    Akizungumza na Centre Spread, Senga alisema alipata fursa hiyo ya kumpiga busu wakati wakiigiza filamu matata ya Pishu iliyoandaliwa na Kajala Entertainment, itakayoingia sokoni Mei Mosi, ambapo alisema anajikubali katika filamu hiyo ambayo anaamini itavunja watu mbavu.
     
    “Wewewee umpige busu Kajala utashindwa kulala kweli jamani,yaani nilishtuka kumeshakucha kabisa lakini pamoja na yote mimi ni mchekeshaji ila kwa filamu ya Pishu nimeinua mikono,” alisema Senga.
     

    TAZAMA TRAILER YA FILAMU MPYA YA PISHU - KAJALA ENTERTAINMENT PRESENTS, KUWA MADUKANI KUANZIA TAREHE 1.05.2015 

    more »

    Wednesday, 22 April 2015

    Tamko La Jeshi La Polisi Pamoja Na Video Ya Tukio Zima La Majambazi Yaliyonaswa Jana Jijini Dar Baada ya Kumpora Mzungu



    Watuhumiwa wanne wamekamatwa jijini Dar es Salaam katika makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel ya Serena baada ya kumpora raia wa kigeni wakiwa na gari dogo rangi ya kijivu yenye nambari za usajili T787 DBU Toyota Cienta.

    Hivi karibuni kumeibuka wimbi la wahalifu kuwapora pesa na vitu vya thamani kama mikufu, bangili, hereni pia pete na vitu mbalimbali vya thamani raia wa kigeni na akina mama ambao hupenda kutembea na pochi. Wahalifu hawa hutumia gari dogo ambalo mara kwa mara hubadilishwa namba zake za usajili na wakati mwingine gari hili wanalitumia kama Tax bubu.

    Leo (jana) tarehe 21/04/2015 majira ya saa 09:00 asubuhi katika eneo la Posta Mpya watuhumiwa hawa walimdangavya bwana CEES S/O JAN CONIJN, Miaka 27, raia wa Uholanzi aliyetaka kufika Klabu ya Leaders kwamba wangempeleka eneo hilo kwa kutumia gari tajwa hapo juu. Baada ya kuondoka na dereva kila baada ya mita 200 dereva huyo alikuwa anasimamisha gari na kuongeza mtu mwingine kama abiria hadi walipotimia wote wane.

    Walimpeleka hadi maeneo ya Kinondoni kwa Manyanya na walipofika eneo hilo walimweleza wazi kuwa wao ni wahalifu na walimtaka awapatie pesa vinginevyo wangemuua. Aliwapatia pesa zote alizokuwa nazo Tshs 75,000/= lakini hawakuridhika ndipo walipomtaka awapatie kadi ya benki (ATM CARD) na nambari za siri (Pass Word).

    Baada ya tukio hilo wakamtupa karibu na Hospitali ya Mwananyamala na wao wakageuza gari kurudi katikati ya mji. Wakati tukio hilo linatokea raia wema walishuhudia na kutoa taarifa kwa Polisi. Polisi walifuatilia haraka na kuweka mtego uliowanasa watuhumiwa wote katika eneo la makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel ya Serena.

    Majina ya watuhumiwa waliokamatwa ni:

    1. SALUM S/O SAID MTUMWA @ MARO, Miaka 25, Mkazi wa Chang’ombe Bora.

    2. ALEX S/O INNOCENT MANGUKA @ MAKA, Miaka 30, Mkazi wa Kimara Temboni.

    3. MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, Miaka 27, Mkazi wa Mwananyamala.

    4. STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING, Miaka 32, Mkazi wa Mwananyamala.

    Walipopekuliwa watuhumiwa hawa walikutwa na simu mbalimbali za mkononi zipatazo 11 ambazo zinachunguzwa kuhusiana na mbinu ya uhalifu wanaoutumia. Pia ilikamatwa ATM CARD iliyochukuliwa kwa mlalamikaji kabla watuhumiwa hao hawajaitumia. Aidha gari namba T787 DBU Toyota Cienta linashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.

    Miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa, wawili ambao ni MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, na STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING, tayari wanazo kesi nyingine mahakamani na wako nje kwa dhamana.

    Sambamba na tukio hili oparesheni ya kuwakamata wahalifu wengine wenye mtindo huu wa kuwapora wageni au wakina mama wenye mikoba inaendelea na tunawaomba wananchi waonyeshe ushirikiano wa kutosha ili kutokomeza vitendo hivyo viovu. Aidha hakuna silaha yoyote iliyotumika au kukamatwa kama ilivyoripotiwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

    S. H. KOVA,
    KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
    DAR ES SALAAM.



    more »

    Al-Shabaab Wakubali Kuhusika na Mlipuko Mogadishu

    Kundi la kigaidi Al-Shabaab la nchini Somalia limetangaza kuhusika na mlipuko wa bomu la
    kutegwa kwenye gari uliotokea jana katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

    Aidha, Shirika la habari la at-Tadhamun la nchini Libya, limemnukuu kiongozi wa kundi hilo Abdul Aziz Abu Mus’ab akisema kuwa kundi hilo ndilo lililohusika na mlipuko huo ambao uliwaua watu 10.

    Hata hivyo, Kwa siku za hivi karibuni wanamgambo hao wamezidisha mashambulizi nchini Somalia na
    nchi jirani kama Kenya kwa lengo la kutaka masharti yao yafatwe.

    more »
    © 2015 THE CIRCLE TV.