Kundi la kigaidi Al-Shabaab la nchini Somalia limetangaza kuhusika na mlipuko wa bomu la
kutegwa kwenye gari uliotokea jana katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.
Aidha, Shirika la habari la at-Tadhamun la nchini Libya, limemnukuu kiongozi wa kundi hilo Abdul Aziz Abu Mus’ab akisema kuwa kundi hilo ndilo lililohusika na mlipuko huo ambao uliwaua watu 10.
Hata hivyo, Kwa siku za hivi karibuni wanamgambo hao wamezidisha mashambulizi nchini Somalia na
nchi jirani kama Kenya kwa lengo la kutaka masharti yao yafatwe.
About the Author
0 comments: